Friday, June 9, 2017

NJIA ZITAKAZO KUJENGEA MSINGI MZURI WA MALI KATIKA UMRI WA 20+




Tabia zitakazo kusaidia kutumia na kutunza fedha kwa umakini,tabia hizi zitakufanya upate msingi bora utakapo fikia umri mkubwa

Tunajua umri wa miaka 20+ ni mzuri wa kujenga maisha,umri huu umejaa furaha na majaribio.Siku hizi umri  huu umekua na changamoto mno zikiambatana na kutengeneza kutengeneza elimu ,kutafuta ajira na wengine kulipa ada mikopo ya ada za shule.Maamuzi utakayofanya ukiwa na miaka 20+ ndio yatakayopelekea matokeo ya uchumi wako katika kipindi chako chote.
"Maisha ni muda" Huwezi endelea na kipato chako kilekile mpaka uzeeni,ili kutimiza ndoto zako jaribu kufanikiwa mapema iwezekanavyo.
Njia hizi zitakazo kufanya kutimiza ndoto zako za kuwa tajiri ukiwa na umri mdogo ni hizi hapa..

1.Tengeneza mpango wa fedha.
Je una mpango gani na mshahara?.Je unahitaji kuwa na kiwango gani cha pesa benki ukifikisha miaka 40?.Je unahitahi kustahafu ukiwa na umri gani?.Haya ni maswali unahiatajika kujiuliza kama unahitaji kujenga utajiri.Majibu hayo muhimu  ndio huitwa malengo.Jaribu kuweka mikakati thabiti kufikia malengo yako ilia kutengeneza mafanikio yako.

2.Lipa madeni.
Kama bado unalipa deni lako la ada ya shule jitahidi kukamilisha,lakini usijisikie vibaya kwa kuwa ndo limekupa mwanga wakupata njia ya mafanikio.

 3.Chagua rafiki sahihi.
Tunajua nguvu za marafiki,rafiki anaweza kukuongoza katika mafanikio pia anaweza kukuongoza katika uharibifu.Inatupasa kutafta marafiki sahihi kutusaidia kufikia malengo yetu.Je ujawahi fuata mkumbo kufanya jambo usilotegemea kwa kufuata vishawishi vya vikundi rika?.Basi jifunze kusema hapana kwa jambo lisilokua la maana,husiogope kuonekana mshamba kwa wenzako.

4.Tafuta mpenzi sahihi.
Mpenzi au mchumba anaweza kuwa na nguvu zaidi ya vikundi rika kukushawishi kufanya jambo fulani linaweza kuwa jema au baya.Tafuta mpenzi au mchumba sahihi anayeweza kukushauri vyema na kukutia moyo katika jambo jema.

5.Chagua taaluma/fani inayolipa zaidi.
Kama unahitaji kujifunza zaidi basi jifunze fani inayolipa na iliyo kwenye soko la ajira.Kuna fani zingine zinalipa zaidi mshahara wake unalipa na fani zingine mshahara wake ni mdogo sana.Jaribu kutathmini juu hilo kulingana na malengo yako ya baadae.


6.Fanya kazi unayoifurahia.
Mwanadamu ili kufanikiwa ni lazima afanye kazi anayoipenda.Jitahidi kutafuta kazi unayoipenda si kutafuta kazi yeyote inayokulipa,ili kufanya kazi kwa bidii unahitaji kufanya ile unayoipenda. 


7. Fanya jambo unaloweza.
     Je hufanyaje kama bado ujapata jambo unalopenda? usiogope.Unaweza fanya jombo unaloweza zaidi lile ambalo unaloujuzi nalo zaidi.Kila mwanadamu katika kuishi hapa duniani kuna jambo kalijifunza na kulifahamu zaidi,unaweza kuta mtu ni mwalimu lakini naweza kusuka zaidi, au mtu ni mwalimu lakini anweza uongozi.Basi chagua kufanya lile jambo unaloweza zaidi.
8.Kujitoa kupitia safari yote ya kuboresha fani.
Fani inahitaji malezi lazima uwe na moyo wa kujitoa kutafuta elimu na uzoefu pia.Umri huu wa miaka 20+ ndo umri wa majaribio kupata au kukosa,ukiwa na umri huu bado una nguvu na ujasiri wa kutosha kupitia changamoto zote katika safari yako.Kama umeajiriwa jitahidi kuongeza uzoefu wako katika taaluma hiyo.

  10.Usione shaka kuomba kupandishwa cheo.
 Katika miaka ya 20+ kama umefanikiwa kuajiriwa muda murefu usiogope kuomba kupandishwa cheo kwa kuwa ithakusaidia kuongeza kipato pia kutengeneza mahusiano na watu wengine wengi watakao mkusaidia kimawazo pia kiuchumi.
11.Acha kazi kama haikusaidii kufikia malengo yako unayoyategemea.
Kama ajira huliyopo haikupi matumaini ya kufikia malengo uliyopanga kuyafikia hakuna budi kuiacha na kutafuta nyingine itakayo kusaidia kufikia malengo yako.
12.Patania mshahara.
Kama unaomba ajira ya ndoto zako ukiwa katika mahojiano usisahau kukubalia na mshahara unaokidha haja zako.

13.Chunguza matumizi yako ya pesa.
  Je wajua fedha zako zinatumikaje kila mwezi? kila senti? 
Viatu hivi vizuri mara ngua hii nzuri mara chakula kidogo,mambo haya hugharimu pesa ndogondogo lakini mwisho baada ya kujumuisha ndipo akiba yako inapo isha bila habari.

14.Andaa bajeti yako ya matumizi.
Kila mtu anajua ili kutunza pesa ni lazima uwe makini wakati wa kupanga bajeti na katika kuitekeleza hiyo bajeti.Huwa ni vigumu sana kuitekeleza bajeti kwa kuwa ni kujinyima vile unavyoona ni vizuri lakini si vya muhimu kwa muda huo.
15.Acha tabia na mazoea yote mabaya.
Watu wengi wamefilisika kwa kupenda anasa ambazo zimekuwa kama mazoea ni ngumu kuzibadilisha.Na hii bila  kushughulikia uwezi fanikiwa katika maisha mfano wa tabia hizi mbaya  ni kama vile ulevi,uasherati ulafi nk.Je ushawahi kufanya hesabu za gharama unazotumia kwa mambo kama hayo?.Aha tabia hizo utafanikiwa.
16. Patania bei ya bidhaa.
Unapo enda kununua bidhaa lazima ujue kuzungumzia bei kwa kua wafanya biashara huuuza bidhaa kwa bei ya juu kuliko uhalisia,kabla kununua bidhaa yeyote unahsuriwa uwe tayari unajua bei yake kabla.Itakusaidia sana katika kupunguza matumizi yako ya fedha na kuboresha maisha yako.

17.Wekeza mafao ya uzeeni.
Sasa hivi ni kijana unayo afya na nguvu pia jitahidi kuwekeza angalau kidogo ili kuja kukuokoa uzeeni pindi nguvu na afya yako itakapo anza kudorora.
18.Weka fedha zako katika mfuko wa kibenki (money market account or CD)
Hiki ni kendo cha kuhifadhimpesa zako katika mfuko wa benki ambao unaruhusiwa kuweka zaidi ya kutoa kwa muda fulani,hii husaidia kukupatia faida pindi muda kutoa unapofika.Hii haitakufanya kuwa tajiri ghafla laikini itakusaidia kuhifadhi pesa zako na kukuepusha na matumizi yasiyo ya lazima.
19.Wekeza katika soko la hisa.
Soko la hisa ni soko ambalo mfanyabiashara anaweza kuwekeza pesa zake katika kampuni fulani na baadaye kupata faida kwa kugawana faida kulingana na kiasi alicho kiwekeza.Hii inaweza kunufaika au kupata hasara,hurusiwi kuuza hisa zako mpaka muda kufika.

20.Fikiri kuwa na makazi yako sahihi.
Ni vyema kuwa na makazi yako kwa kuwa huaidia kupunguza gharama za kuishi mfano kulipa kodi ya pango,na gharama zingine zisizo kuwa za msingi.Hii itakupelekea kupunguza na gharama za maisha na kuongea fedha za ziada.

21.Anzisha biashara.
Je unafikiria kutajirika?.Zinduka ajira pekee haitoshi jaribu kuongeza  kipato kwa kuanzisha biashara nyingine.Ujasiriamali si wa kila mtu lakini ndio chanzo cha kuweza kuendesha na kupanga maisha yako ya kifedha baadae.Usiogope kupoteza fadha zako kwa kuanzisha biashara,jaribu kuenenda na fursa ili kufanikiwa zaidi.
Usisahau kulike share na kutoa maoni katika ukurasa huu
pia endelea kuwa na katika makala zijazo


Friday, June 2, 2017

MAFANIKIO.JIFUNZE NJIA ZA KUPATA CHOCHOTE UNACHOKITAKA KATIKA MAISHA.



MAFANIKIO.JIFUNZE NJIA ZA KUPATA CHOCHOTE UNACHOKITAKA KATIKA MAISHA.


Timiza malengo yako leo.

Je kipi tukifanye kutimiza malengo yetu?.Kila mwanadamu ana jambo anatamani kulitimiza au kulipata,kuna vitu vingi hutukwaza na kukata tamaa kufikia malengo yetu.Mambo haya yamekua kikwazo katika maisha yetu,yametunyima furaha na amani ya pia.Kila mmoja wetu anatamani apate mtu wakusaidia lakini wengi hawajapata,jukumu la kutimiza limebaki kwao peke yao.Kama ni miongoni mwa watu wanaohitaji msaada jumuika name katika makala hii,nakuahidi ukimaliza kujifunza mambo haya lazima upate maarifa ya kupata jambo lolote utakalo.Basi jiunge nami tuangazie njia hizi zitakokufanya uweze kupata jambo la matamaio yako.

 


Njia #1


Tazamia kujitole,si motisha


         Usiangalie faida kwanza tazamia kujitoa kwa kuwa huwezi anza leo leo ukapata faida,watu wengi wameacha biashara walizokua wanazifanya kwa kuwa hawakupata faida,ili biashaea ifanikiwe inahitaji ujitoe sadaka wewe huku ukiwekeza mpaka ikomae ndo uweze faidi hiyo faida.

 


Njia ya #2


Tafuta maarifa kwanza, na si mafanikio


 Mafanikio huletwa na maarifa,jifunze jambo lako unalotaka kulitimiza unaweza kuwa biashara nk.Tafuta elimu ukilichunguza jambo hilo hii hukusaidia kukwepa hasara zisizokua za lazima.Maarifa haya hupatikana kwa kusoma majarida,vitabu au kwa kujifunza watu waliokutanguliz katika jambo hilo.

 


Njia ya #3


Fanya safari yako ya furaha.


Jambo lolote lifanywalo kwa furaha hufanikiwa zaidi,jifunze kujipa furaha peke yako kwa kuwa furaha hileywayo kwa vitu haidumu.Ukifanya safari yako ya kutimiza malengo yako ya furaha itakusaidia kukutia moyo na nguvu za kushinda vikwazo.Epuka msongo wa mawazo na uoga huku ukiwa katika safari hiyo utaishia kuanguka.

 


Njia ya # 4


Epuka fikra za kushindwa.


Fikra hupelekea hisia na  hisia hukupelekea namna gani huichukulie kazi yako.Unazo fikra aina mbili katika ufahamu wako na unayo chaguo moja lakulifuata , ya kwanza ni hupelekea hisia zako kukwa na kushindwa(uoga,wasiwasi),ya pili hupelekea hisia zako kupanda na kusonhga mbele.

 


Njia ya #5


Tumia uwezo wako wa kimawazo(imagination power).


Baada kufanikwa kudhibiti fikra hasi,jambo linalofuata ni hili la kutumia uwezo wako wa kimawazo kuwaza na kutengeneza picha ya  hatua na njia zitakofuata katika safari yako.Hi hukusaidia kukupa nguvu ya kusonga mbele na maarifa yatakayotumika kutimiza hatua hizo.

 


Njia ya #6


Acha kuwa mwema sana kwako.


Utajuaje kuwa uko sahihi?,jichunguze pia jijaribu.Mwanadamu huweza amini kuwa yuko sahihi muda wote ila ukweli tunakoseaga muda mwingine.Ili kujijua kwamba jambo unalolifanya ni jema jichunguze jipe changamoto.Ikiwezekana ruhusu changamoto kwa watu wengine.

 


Njia ya#7


Kushinda uharibifu.


Katika hatua za kufikia malengo kuna mambo ya kukatisha tama tena ya uharibifu.Mambo haya muda mwingine hukufanya kuanguka,jifunze kushikilia lile jema na kuacha lile lisilo na faida.Jitahidi kutumia muda vyema.

 


Njia ya #8.


Usitegemee wengine.


Hateneae cha nduguye hufa masikini.Msemo huu wa zamani una maana kubwa sana,ili kufanikiwa ni lazima ujitahi kuweka mipango yako binafsi ya kutekelezeka si kutegemea watu.Jipimie mzigo ambao una uwezo nao kuubeba.

 


Njia ya #9 

Mipango.


Je kuna jambo lisilohitaji mipango?.Kama hapana kwanini husiandae mpango madhubuti katika malengo yako?.Lazima leo ujue utafanya nini ,kesho pia nk.

 


 Njia ya #10 

Jiepushe na kuchoka.


Unapoanza safari usifikiri kuchoka na kuahirisha kazi balia pambana na jukumu hilo mpaka hutakalo lifikisha mwisho.Hutakapo choka tu ndo mwisho wa hatua zako.


        Mpaka hapoa nikutakie mafanikio mema katika kaufanikisha malengo yako,nikushauri uendelee kusoma makala hii na kuitafakari zaidi.Tuungane tena katika makala zijazo ahsante.

Thursday, June 1, 2017

BIASHARA UNAZOWEZA KUANZISHA HUKU BADO UKIWA KWA MWAJIRI WAKO.

  USIBWETEKE NA AJIRA JARIBU BIASHARA HIZI

Fahamu siku hizi ajira hazina uhakika mno na pia ajira nyingi hazilipi kipato cha kutosha kukizi mahitaji,kwa maana  hiyo pia ukiwa umeajiriwa ni vyema kuanzisha biashara nyingine itakayo weza kukulinda wakati ukiwa umeachishwa kazi au ukiwa umaendelea na kazi.

Baadhi ya biashara hizo zitakozo kuokoa husiadhirike ni pamoja na ...........
            Biashara ya mtandao(network marketing).
Hii ni biashara ambayo unaweza kuifanya kwa muda mchache kwa siku au kwa wiki na ukaanza kujitengenezea kipato hata kama kwa sasa bado umeajiriwa. Kupitia biashara hii wewe unakuwa msambazaji wa huduma au bidhaa kwa njia ya kuwaambia wengine uzuri wa bidhaa au huduma zile na wanaponunua wewe unapata kamisheni. Kuna faida nyingine nyingi kupitia biashara hii kama kuweza kutengeneza timu kubwa na ikakuongezea kipato kikubwa.
Kama unataka kufanya biashara ya aina hii jifunze kwanza kwa undani kwa kujisomea wewe binafsi kisha chagua kampuni unayoweza kufanya nayo na jiunge ili uanze kujenga biashara yako. 
    
                Kuwa mkufunzi binafsi.
Kama kuna ujuzi wowote ambao unao, basi jua kuna watu ambao pia wanauhitaji. Wewe unaweza kuwa mkufunzi binafsi kwa ule ujuzi ambao unao. Kwa mfano kama wewe ni mwalimu, basi unaweza kufanya biashara ya kuwa mwalimu binafsi kwa watoto ambao wazazi wao wana uwezo wa kulipia gharama ya juu kidogo. Wewe unakwenda kuwafundisha watoto hao majumbani kwao. Unatoa huduma nzuri na unahakikisha watoto wanaweza kufaulu vizuri.
Kama unataka kufanya biashara hii, chagua watoto wa aina gani unataka kufundisha, kisha angalia katika watu unaowafahamu ni wangapi wenye watoto wanaoweza kufaidi huduma zako. Tafuta wachache wa kuanza nao hata kwa gharama za chini, fanya nao kazi vizuri na kama watafurahia waombe wazazi wao wakutambulishe kwa marafiki zao ambao wanaweza kufaidika na huduma unayotoa.

              Ushauri wa kitaalamu.

Kwa kazi yoyote ambayo unaifanya, wewe una utaalamu fulani. Utaalamu huo unaweza kuwasaidia watu wengi sana ambao hawajui pa kuupata. Kama wewe ni daktari, unaweza kuwa unawapa watu ushauri kuhusu afya zao, wapo wengi sana wanaohitaji ushauri ila hawajui kama unaweza kupatikana, tena kwa bei rafiki kwao. Kama wewe ni mwanasheria uliyeajiriwa, unaweza kuwa unatoa ushauri wa kisheria kama biashara yako ya pembeni.
Kama unataka kuingia kwenye biashara hii ya kutoa ushauri wa kitaalamu, jua ule utaalamu ambao unao, kisha angalia ni watu gani wanaweza kunufaika na ushauri wako kisha tafuta wachache wa kuanza nao. Endelea kutoa huduma hii ya ushauri ukilenga kujenga jina na baadae unaweza kutoza gharama au kuongeza gharama kama ulianza na kidogo.
   
                 Huduma za kitaalamu.Hii ni tofauti na ushauri wa kitaalamu, hapa unatoa huduma kabisa. Kwa mfano kama wewe ni mhasibu uliyeajiriwa, unaweza kuanzisha biashara yako ya pembeni ya kutoa huduma za kihasibu kwa biashara ndogo ndogo. Wafanyabiashara wengi wadogo hawawezi kumudu gharama kubwa za kupata huduma za uhasibu, kama wewe unaweza kuwaandalia mahesabu yao kwa gharama ambayo wanaweza kuimudu, unaweza kutengeneza biashara kwenye eneo hilo. Kama wewe ni mwanasheria unaweza kutoa huduma za kisheria kwenye jamii kwa gharama ambazo ni rafiki. Kwa mfano kuandalia wenye nyumba mikataba ya upangishaji, kuandalia wafanyabiashara wadogo mikataba ya uajiri, kuwaandalia watu mikataba ya kibiashara na kadhalika. Kuna taasisi nyingi zinafanya hivi lakini zinawafikia wateja wakubwa tu, wewe unaweza kuanza na wateja wadogo na ukajenga biashara yako hapo.
Kama unataka kuingia kwenye biashara hii ya huduma za kitaalamu, jua ile huduma ambayo unaweza kutoa na anza na wateja ambao hawajafikiwa na watoa huduma waliopo. Tengeneza jina lako kwa kutoa huduma nzuri na kuza biashara yako kuanzia hapo.
 Huduma za kitaalamu.
 
Blog unaweza kuitumia kwa biashara zote ambazo tumejadili hapo juu. Unaweza kuitumia kwa kutoa ushauri wa kitaalamu. Kama wewe ni daktari unaandika kuhusu mambo ya afya. Kama wewe ni mtaalamu wa rasilimali watu unaweza kuitumia kuandika kuhusu sifa za kuajiriwa, kudumu kazini, kupandishwa cheo na mengine mengi. Kupitia yale unayoandika unaweza kutengeneza hadhira ambayo inakufuatilia na baadae ukageuza blog yako kuwa biashara kwa kutoza huduma unazotoa, kuweka matangazo au kuuza vitu vyako vingine.
       Nakushukuru ndugu mpenzi msomaji nikushukuru kwa kuwa pamoja nami,usikose makala zingine tamu zinazoendelea kuandaliwa

Tuesday, May 30, 2017

BIASHARA NDOGO ZA MAJUMBANI ZITAKAZO KUTOA KATIKA UMASKINI



JE WAJUA BIASHARA ZA MAJUMBANI  UNAZOWEZA KUANZISHA KWA MTAJI MDOGO?

                    Kama wewe ni mwajiriwa na umezichoka  kero na manyanyaso ya bosi wako,Je unahitaji kuwa bosi wako mwenyewe? Ungana nami katika makala hii uweze kuzijua biashara hizi ndogondogo zinazohitaji mtaji mdogo na kukupa faida kubwa.Wazo la kuanzisha biasharea majumbani ni wazo zuri linalopunguza gharama za uendeshaji na kukupelekea kunufaika zaidi.Biashara hizi hupelekea kupunguza tatizo la ajira pia husaidia wanawake kuepukana na unyanyasaji kutoka kwa waume zao.Badili muda wako wa kukuaa nyumbani kuzalisha kipato,Wazo la kuwa mwajiri wako mwenyewe ni jambo rahisi linalohitaji nidhamu ya hali ya juu sana ,kujituma na kujitambua.Kujiajiri nyumbani kuna faida nyingi kama kuepusha kupoteza muda barabarani,na gharama za nauli nk.Pia biashara hizi zinaweza kukusaidia kukuwezesha kulipia gharama za maisha kama vile kulipa kodi ,gharama za malezi nk.

Kabla ya kuanza biashara yako ya nyumbani kuna mambo mawili matatu ya kutazama

           Jambo la kwanza

 Fanya unachopenda.

Ili kuweza kumudu biashara yako nilazima uchague biashara unayoipenda.Jambo lolote unalopenda ndilo utakalolifanaya kwa moyo zaidi.Watu wengi waacha biashara kwa kuwa walifanya chaguo lisilo sahihi,hivyo kuwafanya kufanya pasipo bidii na uvumilivu pia,Jitahidi kutafuta biashara unayoipenda zaidi hitakusaidi kufanikiwa zaidi.

            Jambo la pili

 Je unayo mtazamo sahihi?.

Ili kufanikiwa ni lazima kuwa na mtazamo chanya wa jambo hilo.Mtazamo chanya hukupa nguzu za kufanya jitihada chanya kufikia malengo yako,jitahidi kabla yakuanza biashara yako uwe tayari kifikra na kimwili katika jambo hilo.Mtazamo chanya pia hukupa uvumilivu katika safari yako kuelekea katika mafanikio,hutakatishwa na kikwazo chochote.


             Jambo la tatu

 Kujenga mipango na mikakati ya kuanzisha biashara yako.

“Mali bila daftari huisha bila habari” msemo huo pia hutumika katika biashara,biashara ambayo haijaanzishwa kwa mipango na mikakati huanguka bila habari.Kabla ya kuanzisha biashara hakikisha unaijifunza kwanza biashara hiyo kabla,kwa kupitia vitamu na watu waliofanikiwa zaidi.Baada ya kufahamu biashara hiyo weka mikakati na mipango itakayokufanya kusonga mbele zaidi bila kukwama bila kusahau sheria na kununi bora zitakazo kuongoza wewe na pia kama hutaitaji wafanya kazi.


BAADA YA KUJIFUNZA HAYO KARIBU TUJIFUNZE BIASHARA HIZO ZA MAJUMBANI


Tutaanza moja moja kwa moja kujifunza biashara hizo yakwanza mpaka ya mwisho

            Kutengeneza na kuuza bidhaa za chakula

Kutengeneza bidhaa za kula majumbani pia mahotelini nk na kuuza mfano biskuti,keki,
Kupata mapishi yako favorite na kuuza, kama vile biskuti, vetkoek, koeksisters, muffins, keki, jams, crips nk huhitaji vifaa vichache na pia vya gharama ndogo vya mapishi.Biashara hii huitaji gharama ndogo ya kuanzia na pia bidhaa hizi huwa na wateja wengi kwa kuwa ni vya bei nafuu na hupendwa na watu wengi.Nikushauri na biashara ndogo ili kuweza kuimudu na kujenga faida kubwa mapema.

           Huduma za kompyuta/computer design.

Kama una kompyuta na vifaa vingine kama vile printer kamera nk,unaweza banzisha huduma za stetionary na kubandika vipeperushi vya matangazo ili kuvutia biashara.Biashara hii noi nzuri na hulipa pale unapokua karibu na shule au ofisi mbalimbali ambazo huhitaji huduma hizo,pia unaweza tengeneza kadi za sherehe na matukio mbalimbali.

         Kupiga picha
Kama unauwezo wa kupiga picha na tayari unayo kamera nzuri, unaweza kuajiri mwenyewe tofauti na kupiga  piga picha za harusi, matukio kama vile siku ya kuzaliwa.unaweza fungua studio yako nyumbani.


            Unaweza kuwa mwalimu.

Ualimu umegawanyika mara nyingi sana,unaweza kusoma fani fulani na kuanza kufundisha wanafunzi wako fani hiyo kama vile ushonaj,musiki na vingine kama hivyo,pia unaweza wafundisha fani nyingine ambazo unazo hata kama ujazisomea lakini unazimudu kama vile uchongaji au ususi.Unaweza jitolea kufundisha bure au kwa bei nafuu kwa muda ili kupata jina.


           Unaweza kua mshonaji.

Kama unauwezo wa kushona au kutarizi nguo na vifaa unavyo basi nkushauri uanze kutumia taaluma yako vizuri kwa kuanza kazi mapema mno,tumia uwezo wako wote katika kukamilisha jambo hilo.

Kituo cha kulea watoto (child care center).
Kwa sababu ya wazazi kubanwa na majukumu ya kila siku,huhitaji watoto wao wapate malezi.Baada ya matendo maovu dhidi ya watoto kuongezeka kupelekea wazazi kupeleka watoto wao  katika vituo hivyo.Kituo hichi ni rahisi kukianzisha kwa kua mahitaji yake ni machache na kukupa faida kubwa mno.



Ghala la kimtandao.(E-Commerce stores).

Unaweza anzisha wigo wa kimtandao mfano JUMIA ,ZOOM TZ,KUPATANA nk na  kuwapa fursa watu kuuza na kununua bidhaa kama vile magari,viwanja,nyumba,vitabu,mavazi  nk  kwa kuwatoza pesa ndo sana.Ndugu mpenzi msomaji naamini makala hii imekuasidia,mpenzi msomaji wangu nichukue nafasi hii kukushukuru nikuombe uendelee kubaki nasi pia usisahau kutoa maoni na kusambaza pia wengine wanufaike na elimu hii ahsante


NJIA ZITAKAZO KUJENGEA MSINGI MZURI WA MALI KATIKA UMRI WA 20+

Tabia zitakazo kusaidia kutumia na kutunza fedha kwa umakini,tabia hizi zitakufanya upate msingi bora utakapo fikia umri mkubw...