MAFANIKIO.JIFUNZE NJIA ZA KUPATA CHOCHOTE UNACHOKITAKA KATIKA MAISHA.
Je kipi tukifanye kutimiza malengo yetu?.Kila mwanadamu ana jambo anatamani kulitimiza au kulipata,kuna vitu vingi hutukwaza na kukata tamaa kufikia malengo yetu.Mambo haya yamekua kikwazo katika maisha yetu,yametunyima furaha na amani ya pia.Kila mmoja wetu anatamani apate mtu wakusaidia lakini wengi hawajapata,jukumu la kutimiza limebaki kwao peke yao.Kama ni miongoni mwa watu wanaohitaji msaada jumuika name katika makala hii,nakuahidi ukimaliza kujifunza mambo haya lazima upate maarifa ya kupata jambo lolote utakalo.Basi jiunge nami tuangazie njia hizi zitakokufanya uweze kupata jambo la matamaio yako.
Njia #1
Tazamia kujitole,si motisha
Usiangalie faida kwanza tazamia kujitoa kwa kuwa huwezi anza leo leo ukapata faida,watu wengi wameacha biashara walizokua wanazifanya kwa kuwa hawakupata faida,ili biashaea ifanikiwe inahitaji ujitoe sadaka wewe huku ukiwekeza mpaka ikomae ndo uweze faidi hiyo faida.
Njia ya #2
Tafuta maarifa kwanza, na si mafanikio
Mafanikio huletwa na maarifa,jifunze jambo lako unalotaka kulitimiza unaweza kuwa biashara nk.Tafuta elimu ukilichunguza jambo hilo hii hukusaidia kukwepa hasara zisizokua za lazima.Maarifa haya hupatikana kwa kusoma majarida,vitabu au kwa kujifunza watu waliokutanguliz katika jambo hilo.
Njia ya #3
Fanya safari yako ya furaha.
Jambo lolote lifanywalo kwa furaha hufanikiwa zaidi,jifunze kujipa furaha peke yako kwa kuwa furaha hileywayo kwa vitu haidumu.Ukifanya safari yako ya kutimiza malengo yako ya furaha itakusaidia kukutia moyo na nguvu za kushinda vikwazo.Epuka msongo wa mawazo na uoga huku ukiwa katika safari hiyo utaishia kuanguka.
Njia ya # 4
Epuka fikra za kushindwa.
Fikra hupelekea hisia na hisia hukupelekea namna gani huichukulie kazi yako.Unazo fikra aina mbili katika ufahamu wako na unayo chaguo moja lakulifuata , ya kwanza ni hupelekea hisia zako kukwa na kushindwa(uoga,wasiwasi),ya pili hupelekea hisia zako kupanda na kusonhga mbele.
Njia ya #5
Tumia uwezo wako wa kimawazo(imagination power).
Baada kufanikwa kudhibiti fikra hasi,jambo linalofuata ni hili la kutumia uwezo wako wa kimawazo kuwaza na kutengeneza picha ya hatua na njia zitakofuata katika safari yako.Hi hukusaidia kukupa nguvu ya kusonga mbele na maarifa yatakayotumika kutimiza hatua hizo.
Njia ya #6
Acha kuwa mwema sana kwako.
Utajuaje kuwa uko sahihi?,jichunguze pia jijaribu.Mwanadamu huweza amini kuwa yuko sahihi muda wote ila ukweli tunakoseaga muda mwingine.Ili kujijua kwamba jambo unalolifanya ni jema jichunguze jipe changamoto.Ikiwezekana ruhusu changamoto kwa watu wengine.
Njia ya#7
Kushinda uharibifu.
Katika hatua za kufikia malengo kuna mambo ya kukatisha tama tena ya uharibifu.Mambo haya muda mwingine hukufanya kuanguka,jifunze kushikilia lile jema na kuacha lile lisilo na faida.Jitahidi kutumia muda vyema.
Njia ya #8.
Usitegemee wengine.
Hateneae cha nduguye hufa masikini.Msemo huu wa zamani una maana kubwa sana,ili kufanikiwa ni lazima ujitahi kuweka mipango yako binafsi ya kutekelezeka si kutegemea watu.Jipimie mzigo ambao una uwezo nao kuubeba.
Njia ya #9
Mipango.
Je kuna jambo lisilohitaji mipango?.Kama hapana kwanini husiandae mpango madhubuti katika malengo yako?.Lazima leo ujue utafanya nini ,kesho pia nk.
Njia ya #10
Jiepushe na kuchoka.
Unapoanza safari usifikiri kuchoka na kuahirisha kazi balia pambana na jukumu hilo mpaka hutakalo lifikisha mwisho.Hutakapo choka tu ndo mwisho wa hatua zako.
Mpaka hapoa
nikutakie mafanikio mema katika kaufanikisha malengo yako,nikushauri uendelee
kusoma makala hii na kuitafakari zaidi.Tuungane tena katika makala zijazo
ahsante.
No comments:
Post a Comment