Tabia zitakazo kusaidia kutumia na kutunza fedha kwa umakini,tabia hizi zitakufanya upate msingi bora utakapo fikia umri mkubwa
Tunajua umri wa miaka 20+ ni mzuri
wa kujenga maisha,umri huu umejaa furaha na majaribio.Siku hizi umri
huu umekua na changamoto mno zikiambatana na kutengeneza kutengeneza elimu
,kutafuta ajira na wengine kulipa ada mikopo ya ada za shule.Maamuzi
utakayofanya ukiwa na miaka 20+ ndio yatakayopelekea matokeo ya uchumi wako
katika kipindi chako chote.
|
"Maisha ni muda" Huwezi
endelea na kipato chako kilekile mpaka uzeeni,ili kutimiza ndoto zako jaribu
kufanikiwa mapema iwezekanavyo.
Njia hizi zitakazo kufanya kutimiza
ndoto zako za kuwa tajiri ukiwa na umri mdogo ni hizi hapa..
1.Tengeneza
mpango wa fedha.
Je una mpango gani na mshahara?.Je
unahitaji kuwa na kiwango gani cha pesa benki ukifikisha miaka 40?.Je
unahitahi kustahafu ukiwa na umri gani?.Haya ni maswali unahiatajika
kujiuliza kama unahitaji kujenga utajiri.Majibu hayo muhimu ndio huitwa
malengo.Jaribu kuweka mikakati thabiti kufikia malengo yako ilia kutengeneza
mafanikio yako.
|
2.Lipa
madeni.
Kama bado unalipa deni lako la ada ya
shule jitahidi kukamilisha,lakini usijisikie vibaya kwa kuwa ndo limekupa
mwanga wakupata njia ya mafanikio.
3.Chagua rafiki sahihi.
Tunajua nguvu za marafiki,rafiki
anaweza kukuongoza katika mafanikio pia anaweza kukuongoza katika
uharibifu.Inatupasa kutafta marafiki sahihi kutusaidia kufikia malengo yetu.Je
ujawahi fuata mkumbo kufanya jambo usilotegemea kwa kufuata vishawishi vya
vikundi rika?.Basi jifunze kusema hapana kwa jambo lisilokua la maana,husiogope
kuonekana mshamba kwa wenzako.
4.Tafuta
mpenzi sahihi.
Mpenzi au mchumba anaweza kuwa na
nguvu zaidi ya vikundi rika kukushawishi kufanya jambo fulani linaweza kuwa
jema au baya.Tafuta mpenzi au mchumba sahihi anayeweza kukushauri vyema na
kukutia moyo katika jambo jema.
5.Chagua
taaluma/fani inayolipa zaidi.
Kama unahitaji kujifunza zaidi basi
jifunze fani inayolipa na iliyo kwenye soko la ajira.Kuna fani zingine zinalipa
zaidi mshahara wake unalipa na fani zingine mshahara wake ni mdogo sana.Jaribu
kutathmini juu hilo kulingana na malengo yako ya baadae.
6.Fanya
kazi unayoifurahia.
Mwanadamu ili kufanikiwa ni lazima
afanye kazi anayoipenda.Jitahidi kutafuta kazi unayoipenda si kutafuta kazi
yeyote inayokulipa,ili kufanya kazi kwa bidii unahitaji kufanya ile
unayoipenda.
|
7. Fanya jambo
unaloweza.
Je hufanyaje
kama bado ujapata jambo unalopenda? usiogope.Unaweza fanya jombo unaloweza
zaidi lile ambalo unaloujuzi nalo zaidi.Kila mwanadamu katika kuishi hapa
duniani kuna jambo kalijifunza na kulifahamu zaidi,unaweza kuta mtu ni mwalimu
lakini naweza kusuka zaidi, au mtu ni mwalimu lakini anweza uongozi.Basi chagua
kufanya lile jambo unaloweza zaidi.
8.Kujitoa
kupitia safari yote ya kuboresha fani.
Fani inahitaji malezi lazima uwe na
moyo wa kujitoa kutafuta elimu na uzoefu pia.Umri huu wa miaka 20+ ndo umri wa
majaribio kupata au kukosa,ukiwa na umri huu bado una nguvu na ujasiri wa
kutosha kupitia changamoto zote katika safari yako.Kama umeajiriwa jitahidi
kuongeza uzoefu wako katika taaluma hiyo.
10.Usione shaka kuomba kupandishwa cheo.
Katika
miaka ya 20+ kama umefanikiwa kuajiriwa muda murefu usiogope kuomba kupandishwa
cheo kwa kuwa ithakusaidia kuongeza kipato pia kutengeneza mahusiano na watu
wengine wengi watakao mkusaidia kimawazo pia kiuchumi.
11.Acha
kazi kama haikusaidii kufikia malengo yako unayoyategemea.
Kama ajira
huliyopo haikupi matumaini ya kufikia malengo uliyopanga kuyafikia hakuna budi
kuiacha na kutafuta nyingine itakayo kusaidia kufikia malengo yako.
12.Patania
mshahara.
Kama
unaomba ajira ya ndoto zako ukiwa katika mahojiano usisahau kukubalia na
mshahara unaokidha haja zako.
13.Chunguza
matumizi yako ya pesa.
|
Je
wajua fedha zako zinatumikaje kila mwezi? kila senti?
Viatu hivi
vizuri mara ngua hii nzuri mara chakula kidogo,mambo haya hugharimu pesa
ndogondogo lakini mwisho baada ya kujumuisha ndipo akiba yako inapo isha bila
habari.
14.Andaa
bajeti yako ya matumizi.
Kila mtu
anajua ili kutunza pesa ni lazima uwe makini wakati wa kupanga bajeti na katika
kuitekeleza hiyo bajeti.Huwa ni vigumu sana kuitekeleza bajeti kwa kuwa ni
kujinyima vile unavyoona ni vizuri lakini si vya muhimu kwa muda huo.
15.Acha
tabia na mazoea yote mabaya.
Watu wengi
wamefilisika kwa kupenda anasa ambazo zimekuwa kama mazoea ni ngumu
kuzibadilisha.Na hii bila kushughulikia uwezi fanikiwa katika maisha
mfano wa tabia hizi mbaya ni kama vile ulevi,uasherati ulafi nk.Je
ushawahi kufanya hesabu za gharama unazotumia kwa mambo kama hayo?.Aha tabia
hizo utafanikiwa.
16. Patania
bei ya bidhaa.
Unapo enda kununua bidhaa lazima ujue
kuzungumzia bei kwa kua wafanya biashara huuuza bidhaa kwa bei ya juu kuliko
uhalisia,kabla kununua bidhaa yeyote unahsuriwa uwe tayari unajua bei yake
kabla.Itakusaidia sana katika kupunguza matumizi yako ya fedha na kuboresha
maisha yako.
17.Wekeza
mafao ya uzeeni.
Sasa hivi ni kijana unayo afya na
nguvu pia jitahidi kuwekeza angalau kidogo ili kuja kukuokoa uzeeni pindi nguvu na
afya yako itakapo anza kudorora.
18.Weka
fedha zako katika mfuko wa kibenki (money market account or CD)
Hiki ni
kendo cha kuhifadhimpesa zako katika mfuko wa benki ambao unaruhusiwa kuweka
zaidi ya kutoa kwa muda fulani,hii husaidia kukupatia faida pindi muda kutoa
unapofika.Hii haitakufanya kuwa tajiri ghafla laikini itakusaidia kuhifadhi
pesa zako na kukuepusha na matumizi yasiyo ya lazima.
|
19.Wekeza
katika soko la hisa.
Soko la hisa ni soko ambalo
mfanyabiashara anaweza kuwekeza pesa zake katika kampuni fulani na baadaye
kupata faida kwa kugawana faida kulingana na kiasi alicho kiwekeza.Hii
inaweza kunufaika au kupata hasara,hurusiwi kuuza hisa zako mpaka muda
kufika.
|
20.Fikiri
kuwa na makazi yako sahihi.
Ni vyema
kuwa na makazi yako kwa kuwa huaidia kupunguza gharama za kuishi mfano kulipa
kodi ya pango,na gharama zingine zisizo kuwa za msingi.Hii itakupelekea
kupunguza na gharama za maisha na kuongea fedha za ziada.
21.Anzisha
biashara.
Je
unafikiria kutajirika?.Zinduka ajira pekee haitoshi jaribu kuongeza
kipato kwa kuanzisha biashara nyingine.Ujasiriamali si wa kila mtu lakini ndio
chanzo cha kuweza kuendesha na kupanga maisha yako ya kifedha baadae.Usiogope
kupoteza fadha zako kwa kuanzisha biashara,jaribu kuenenda na fursa ili
kufanikiwa zaidi.
Usisahau
kulike share na kutoa maoni katika ukurasa huu
pia endelea
kuwa na katika makala zijazo
No comments:
Post a Comment