Tuesday, May 30, 2017

BIASHARA NDOGO ZA MAJUMBANI ZITAKAZO KUTOA KATIKA UMASKINI



JE WAJUA BIASHARA ZA MAJUMBANI  UNAZOWEZA KUANZISHA KWA MTAJI MDOGO?

                    Kama wewe ni mwajiriwa na umezichoka  kero na manyanyaso ya bosi wako,Je unahitaji kuwa bosi wako mwenyewe? Ungana nami katika makala hii uweze kuzijua biashara hizi ndogondogo zinazohitaji mtaji mdogo na kukupa faida kubwa.Wazo la kuanzisha biasharea majumbani ni wazo zuri linalopunguza gharama za uendeshaji na kukupelekea kunufaika zaidi.Biashara hizi hupelekea kupunguza tatizo la ajira pia husaidia wanawake kuepukana na unyanyasaji kutoka kwa waume zao.Badili muda wako wa kukuaa nyumbani kuzalisha kipato,Wazo la kuwa mwajiri wako mwenyewe ni jambo rahisi linalohitaji nidhamu ya hali ya juu sana ,kujituma na kujitambua.Kujiajiri nyumbani kuna faida nyingi kama kuepusha kupoteza muda barabarani,na gharama za nauli nk.Pia biashara hizi zinaweza kukusaidia kukuwezesha kulipia gharama za maisha kama vile kulipa kodi ,gharama za malezi nk.

Kabla ya kuanza biashara yako ya nyumbani kuna mambo mawili matatu ya kutazama

           Jambo la kwanza

 Fanya unachopenda.

Ili kuweza kumudu biashara yako nilazima uchague biashara unayoipenda.Jambo lolote unalopenda ndilo utakalolifanaya kwa moyo zaidi.Watu wengi waacha biashara kwa kuwa walifanya chaguo lisilo sahihi,hivyo kuwafanya kufanya pasipo bidii na uvumilivu pia,Jitahidi kutafuta biashara unayoipenda zaidi hitakusaidi kufanikiwa zaidi.

            Jambo la pili

 Je unayo mtazamo sahihi?.

Ili kufanikiwa ni lazima kuwa na mtazamo chanya wa jambo hilo.Mtazamo chanya hukupa nguzu za kufanya jitihada chanya kufikia malengo yako,jitahidi kabla yakuanza biashara yako uwe tayari kifikra na kimwili katika jambo hilo.Mtazamo chanya pia hukupa uvumilivu katika safari yako kuelekea katika mafanikio,hutakatishwa na kikwazo chochote.


             Jambo la tatu

 Kujenga mipango na mikakati ya kuanzisha biashara yako.

“Mali bila daftari huisha bila habari” msemo huo pia hutumika katika biashara,biashara ambayo haijaanzishwa kwa mipango na mikakati huanguka bila habari.Kabla ya kuanzisha biashara hakikisha unaijifunza kwanza biashara hiyo kabla,kwa kupitia vitamu na watu waliofanikiwa zaidi.Baada ya kufahamu biashara hiyo weka mikakati na mipango itakayokufanya kusonga mbele zaidi bila kukwama bila kusahau sheria na kununi bora zitakazo kuongoza wewe na pia kama hutaitaji wafanya kazi.


BAADA YA KUJIFUNZA HAYO KARIBU TUJIFUNZE BIASHARA HIZO ZA MAJUMBANI


Tutaanza moja moja kwa moja kujifunza biashara hizo yakwanza mpaka ya mwisho

            Kutengeneza na kuuza bidhaa za chakula

Kutengeneza bidhaa za kula majumbani pia mahotelini nk na kuuza mfano biskuti,keki,
Kupata mapishi yako favorite na kuuza, kama vile biskuti, vetkoek, koeksisters, muffins, keki, jams, crips nk huhitaji vifaa vichache na pia vya gharama ndogo vya mapishi.Biashara hii huitaji gharama ndogo ya kuanzia na pia bidhaa hizi huwa na wateja wengi kwa kuwa ni vya bei nafuu na hupendwa na watu wengi.Nikushauri na biashara ndogo ili kuweza kuimudu na kujenga faida kubwa mapema.

           Huduma za kompyuta/computer design.

Kama una kompyuta na vifaa vingine kama vile printer kamera nk,unaweza banzisha huduma za stetionary na kubandika vipeperushi vya matangazo ili kuvutia biashara.Biashara hii noi nzuri na hulipa pale unapokua karibu na shule au ofisi mbalimbali ambazo huhitaji huduma hizo,pia unaweza tengeneza kadi za sherehe na matukio mbalimbali.

         Kupiga picha
Kama unauwezo wa kupiga picha na tayari unayo kamera nzuri, unaweza kuajiri mwenyewe tofauti na kupiga  piga picha za harusi, matukio kama vile siku ya kuzaliwa.unaweza fungua studio yako nyumbani.


            Unaweza kuwa mwalimu.

Ualimu umegawanyika mara nyingi sana,unaweza kusoma fani fulani na kuanza kufundisha wanafunzi wako fani hiyo kama vile ushonaj,musiki na vingine kama hivyo,pia unaweza wafundisha fani nyingine ambazo unazo hata kama ujazisomea lakini unazimudu kama vile uchongaji au ususi.Unaweza jitolea kufundisha bure au kwa bei nafuu kwa muda ili kupata jina.


           Unaweza kua mshonaji.

Kama unauwezo wa kushona au kutarizi nguo na vifaa unavyo basi nkushauri uanze kutumia taaluma yako vizuri kwa kuanza kazi mapema mno,tumia uwezo wako wote katika kukamilisha jambo hilo.

Kituo cha kulea watoto (child care center).
Kwa sababu ya wazazi kubanwa na majukumu ya kila siku,huhitaji watoto wao wapate malezi.Baada ya matendo maovu dhidi ya watoto kuongezeka kupelekea wazazi kupeleka watoto wao  katika vituo hivyo.Kituo hichi ni rahisi kukianzisha kwa kua mahitaji yake ni machache na kukupa faida kubwa mno.



Ghala la kimtandao.(E-Commerce stores).

Unaweza anzisha wigo wa kimtandao mfano JUMIA ,ZOOM TZ,KUPATANA nk na  kuwapa fursa watu kuuza na kununua bidhaa kama vile magari,viwanja,nyumba,vitabu,mavazi  nk  kwa kuwatoza pesa ndo sana.Ndugu mpenzi msomaji naamini makala hii imekuasidia,mpenzi msomaji wangu nichukue nafasi hii kukushukuru nikuombe uendelee kubaki nasi pia usisahau kutoa maoni na kusambaza pia wengine wanufaike na elimu hii ahsante


3 comments:

  1. Nimeipenda makala hii mie binafsi nimejitaftia shughuli ya kufanya. Nashona mitandio ile ya kimasai ya shanga ni mfanyakazi ila natumia mda wa ziada kufanya hayo na najipatia pesa. Pia napika keki za matukio mbalimbali. Wamama ambao hamna ajira angalieni changamoto ya watu kukosa mahousegirl na kulifanyika kazi kwa kujiunga kuanzisha daycare

    ReplyDelete
  2. Nimeipenda Sana makala hii I will apply it

    ReplyDelete
  3. We are moving 4ward as a nation, very good ideas

    ReplyDelete

NJIA ZITAKAZO KUJENGEA MSINGI MZURI WA MALI KATIKA UMRI WA 20+

Tabia zitakazo kusaidia kutumia na kutunza fedha kwa umakini,tabia hizi zitakufanya upate msingi bora utakapo fikia umri mkubw...