Mmusi Maimane azuiwa kuingia Zambia
Polisi nchini Zambia wamemzuia kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Afrika kusini kuingia nchini Humo.
Mmusi
Maimane kutoka chama cha Democratic Alliance, alikuwa akitarajiwa
kuhudhuria kesi inayomkabili kiongozi wa upinzani nchini humo Haikande
Hichilema.Bwana Hichilema anashtakiwa kwa makosa ya uhaini baada ya kushindwa kutoa njia kwa msafara wa Rais wa Zambia, hali ambayo inadaiwa kuhatarisha maisha ya mkuu huyo wa nchi.
Kiongozi huyo wa upinzani nchini Afrika kusini Mmusi Maimane amesema amelazimika kurudi nyumbani baada ya maafisa kuingia ndani ya ndege ya Shirika la ndege la Afrika kusini aliyokuwa amesafiri nayo mjini Lusaka, kumvamia na kumnyang'anya simu yake.
Hata hivyo bado hakuna taarifa zozote zilizotolewa na serikali ya Zambia.
No comments:
Post a Comment