Mbinu hizi zitakusaidia kutoka
Nijambo gani linalowafanya watu fulani pekee kufanikiwa?,
jambo gani linalo wahamasisha?.
Vitu hivi vimenifanya kuandika makala hii ili kuwasaidia
watu wenye nia ya kubadili maisha yao lakini hawajui wafanye nini.Zifuatazo ni mambo yanayoweza kukufanya ubadili maisha yako pale
tu utakapo zifahahamu.
UJIAMINI NA
KUJIKUBALI.
Hiyo ni nguvu inayowafanya kusonga mbele kwa kua hujua
thamani yao hiyo huwafanya kujiamini mno na kujikuli pia.Hilo huwafanya kusonga mbele katika mipango yao bila kukubali mtu yeyote
kumrudisha nyuma au kumkatisha tama.
HUWA NA MALENGO, MADHUMUNI NA MAONO SAHIHI.
Maendeleo ya mwanadamu huhitaji mikakati thabiti ili kuweza kutekeleza mipango.Pale mwanadamu anakosa malengo hujikuta akihangaika huku na
huko bila kujua cha kufanya kipi,na hiyo humfanya kukosa au kuchelewa kuapata
mafanikio.Malengo,madhumuni na maono sahihi humpeleka mtukwenye mafanikio moja
kwa moja.
UTAYARI WA KUFANYA KAZI.
Watu wa mafanikio wana shauku ya kufanya kwa bidii
zaidi.Tambua mafanikio huletwa na utayari wako kifikra na kimwili pia, bila kua
tayari kufanya kazi kwa bidii unatemegemea kufanikiwa?Jibu ni hapana lazima
ujitahidi kutoa mwili na akili yako kufanya kazi kwa bidii zaidi.
NIDHAMU.
Tambua mafanikio hujengwa na nidhamu ya halii ya juu lazima
ujifunze kuheshimu wewe na mipango yako,jitahidi kujiagiza kuheshimu maagizo
yako peke ako.
AKILI SHIRIKISHI.
Watu wanaohitaji kua na mafanikio lazima wawe na akili
shirikishi au jumauishi kati ya mawazo
na akili zao.Huamini akili na mawazo yao .Unapokua na akili shirikishi ni
lazima upate mafanikio kwa kua huwezi fanya jambo lilo nje ya mipango yako.
KUJIFUNZA KWA FAIDA.
Kusoma kwa faida ni jimbo zuri sana kama unataka mafanikio
ya haraka,kwa kusoma huko hukupa elimu unayoitaka kukusaidia kutimiza mipango
yako.Mfano unahitaji kufuga kuku wa nyama ni lazim husome na kufuatilia haytua kwa hatua kanuni
za ufugaji bora.Bila kujifunza kwa faida huwezi timiza ndoto zako.
KUJITAMBUA
Kujitambua ni hatua mojawapo kubwa ya mafanikio,ili kupata
mafanikio ni lazima hujue wewe umekuja Dunini kufanya nini.Hukifanya jambo
ambalo unalipenda jua utafanya kwa moyo zaidi na kupata mafanikio zaidi ,kwa msaada kujitambua wewe ninani bofya hapa >> UNADHANI WEWE NI NANI?
Asante kwa kua nami katika makala hii tukutane tena katika makala zingine
No comments:
Post a Comment