JE WEWE WAHITAJI KUBADILIKA NA KUISHI MAISHA YATAKAYO KUPELEKA KATIKA MAFANIKIO?
Leo nakualika tujifunze vitu ambavyo hufanywa na watu wenye uwezo mkubwa kifikra huvifanya.Utamaduni huu ni mzuri pale tutakapo uchukua na kuuishi,tunaweza badili maisha yetu kwa ujumla nakuwa wamafanikio pia katika kipindi hiki tunachoishi hapa duniani.
Watu hawa washindi huwa hawakwamishwi na jambo lolote wanalokutana nalo husonga mbele mpaka wafike walipokusudia.Ili kuwa wamafinikio zaidi hutakiwi kukwama au kusita,pale unapokutana na vikwao,kujikwaa,au kujikwaa katika jambo ulilozamiria fanya katika maisha usitazame nyuma songa mbele.
#2:NIVIONGOZI WA MAISHA YAO WENYEWE..
Hawakubali kuendeshwa na mazingira hujiendesha wenyewe.Ili kuyashinda maisha usikubali kupelekwa na maisha ovyo.Baki na nguvu yako ya kuyaongoza maisha yako.
#3:HUKABILIANA NA CHANGAMOTO.
Huamini kua ili kufanikiwa lazima ukabiliane na changamoto za kila namna bila kukata tamaa.Utamaduni huu ni mzuri kwa kua watu wengi wakikutana na vikwazo huacha walichodhamiria kufanya.changamoto hazina budi kuja na pia huna budi kuzikabili.
#3:HUWA NA FURAHA.
Watu hawa hawaangaiki kufanya mambo wasiyo yaweza kuyafanya, hawakuzi mambo kichwani bila ufumbuzi(hawa complicate) hiyo huwasaidia kupunguza ,msongo wa mawazo,na hiyo huwafanya wenye furaha mda wote.
#5:NI WAKARIMU.
Ukarimu kuwajengea urafiki na watu mbalimbali ,na pia kupata msaada kufankisha mipango yao.
#6:HUJIWEKEKEZA WAO NA NGUVU ZAO.
Hutumia muda wao na nguvu zao kutimiza mipango yao ,si wavivu ni wachapa kazi kwakua hujua wanahitaji kufanikisha ndoto zao.
#7:HUPOKEA JUKUMU LA TABIA ZAO ZA NYUMA.
Hukubali lawama na adhabu ya makosa walio kua wakifanya kabla,Ili kupokea mabadiliko ni lazima utambua makosa yako na kuyadhamiria kuacha.
#8HUFURAHIA MAFANIKIO YA WATU WENGINE.
Tunajua usipofurahia mafanikio yako huwezi pata bidii na wewe ya kupata bali utatafuta njia ya kumrudisha nyuma.
#9WAKO TAYARI KUPOKEA HATA KUSHINDWA.
Kushindwa na kushinda vyote ni matokea.Unaposhindwa usikubali kulala amka jifunze ulikosea wapi ,afu tena anza upya.Mabingwa wa masumbwi hupigwa ila hawaachi mapambano hurudia na kutudia zaidi.
#10:HUFURAHIA MUDA KWA KUKAA PEKE YAO.
Hawaogopi kujitenga na watu hujaribu kupata muda na mahali palipo tulia ili kupata nafasi ya kutafakari.Kukaa peke ako husaidia kupata mawazo mapya ambayo hujenga mipango mipya.
#11:HUJIANDAA KUFANYA KAZI NA KUNUFAIKA NA MATUNDA YAO.
Hafanya kazi wakiamini kwamba dunia haiwapi chochote ,hujitahidi kufanya peke yao wakitamizia mafanikio ya kazi za mikono yao wenyewe.
#12:HUBAKI NA NGUVU MUDA WOTE.
Hawategemei mafanikio ya ghafla hvyo huwafanya wenye nguvu muda wote wakipambana mpaka wapate mafanikio.
#13:HUYAPA MAWAZO YAO THAMANI.
Ili kufanikiwa lazima uamini mawazo yako yanathamani,na hivyo utayaheshimu na kuyafanyia kazi hutayaacha yapite tu.
#14:HUTUMIA NGUVU ZA AKILI ZAO VYEMA.
Watu wenye mafanikio hutumia muda wao vizuri kwa mambo yenye maana na si kupoteza muda.
Ili kufanikiwa ni lazima kupanga ratiba zako vyema ili kupunguza nguvu na muda wakupoteza.
#15:HUFIKIRI MAWAZO CHANYA .
Hutumia ubongo kuwaza mambo chanya kwa kuyaacha yale hasi.Hii husaidia kupata mbinu mpya za ushindi.
#16:HUVUMILIA VIKWAZO.
Ili mtu kufanikiwa lazima uweze vumilia yakukatisha tamaa.Nakuendelea na moyo uleule kutimiza ndoto zao.
#17:NI WAJASIRI.
Ili kufanikiwa lazima uwe na moyo wa kijasiri ,ili uweze kufanikiwa lazima uwe risk taker.
Ndugu mpenzi msomaji nimuombe tu usisome bila kutafakari na pia kufanyia kazi .Huki jaribu kufuata vitu hivyo nakuahidi tegemea mabadiliko makubwa.
.
No comments:
Post a Comment