Thursday, June 1, 2017

BIASHARA UNAZOWEZA KUANZISHA HUKU BADO UKIWA KWA MWAJIRI WAKO.

  USIBWETEKE NA AJIRA JARIBU BIASHARA HIZI

Fahamu siku hizi ajira hazina uhakika mno na pia ajira nyingi hazilipi kipato cha kutosha kukizi mahitaji,kwa maana  hiyo pia ukiwa umeajiriwa ni vyema kuanzisha biashara nyingine itakayo weza kukulinda wakati ukiwa umeachishwa kazi au ukiwa umaendelea na kazi.

Baadhi ya biashara hizo zitakozo kuokoa husiadhirike ni pamoja na ...........
            Biashara ya mtandao(network marketing).
Hii ni biashara ambayo unaweza kuifanya kwa muda mchache kwa siku au kwa wiki na ukaanza kujitengenezea kipato hata kama kwa sasa bado umeajiriwa. Kupitia biashara hii wewe unakuwa msambazaji wa huduma au bidhaa kwa njia ya kuwaambia wengine uzuri wa bidhaa au huduma zile na wanaponunua wewe unapata kamisheni. Kuna faida nyingine nyingi kupitia biashara hii kama kuweza kutengeneza timu kubwa na ikakuongezea kipato kikubwa.
Kama unataka kufanya biashara ya aina hii jifunze kwanza kwa undani kwa kujisomea wewe binafsi kisha chagua kampuni unayoweza kufanya nayo na jiunge ili uanze kujenga biashara yako. 
    
                Kuwa mkufunzi binafsi.
Kama kuna ujuzi wowote ambao unao, basi jua kuna watu ambao pia wanauhitaji. Wewe unaweza kuwa mkufunzi binafsi kwa ule ujuzi ambao unao. Kwa mfano kama wewe ni mwalimu, basi unaweza kufanya biashara ya kuwa mwalimu binafsi kwa watoto ambao wazazi wao wana uwezo wa kulipia gharama ya juu kidogo. Wewe unakwenda kuwafundisha watoto hao majumbani kwao. Unatoa huduma nzuri na unahakikisha watoto wanaweza kufaulu vizuri.
Kama unataka kufanya biashara hii, chagua watoto wa aina gani unataka kufundisha, kisha angalia katika watu unaowafahamu ni wangapi wenye watoto wanaoweza kufaidi huduma zako. Tafuta wachache wa kuanza nao hata kwa gharama za chini, fanya nao kazi vizuri na kama watafurahia waombe wazazi wao wakutambulishe kwa marafiki zao ambao wanaweza kufaidika na huduma unayotoa.

              Ushauri wa kitaalamu.

Kwa kazi yoyote ambayo unaifanya, wewe una utaalamu fulani. Utaalamu huo unaweza kuwasaidia watu wengi sana ambao hawajui pa kuupata. Kama wewe ni daktari, unaweza kuwa unawapa watu ushauri kuhusu afya zao, wapo wengi sana wanaohitaji ushauri ila hawajui kama unaweza kupatikana, tena kwa bei rafiki kwao. Kama wewe ni mwanasheria uliyeajiriwa, unaweza kuwa unatoa ushauri wa kisheria kama biashara yako ya pembeni.
Kama unataka kuingia kwenye biashara hii ya kutoa ushauri wa kitaalamu, jua ule utaalamu ambao unao, kisha angalia ni watu gani wanaweza kunufaika na ushauri wako kisha tafuta wachache wa kuanza nao. Endelea kutoa huduma hii ya ushauri ukilenga kujenga jina na baadae unaweza kutoza gharama au kuongeza gharama kama ulianza na kidogo.
   
                 Huduma za kitaalamu.Hii ni tofauti na ushauri wa kitaalamu, hapa unatoa huduma kabisa. Kwa mfano kama wewe ni mhasibu uliyeajiriwa, unaweza kuanzisha biashara yako ya pembeni ya kutoa huduma za kihasibu kwa biashara ndogo ndogo. Wafanyabiashara wengi wadogo hawawezi kumudu gharama kubwa za kupata huduma za uhasibu, kama wewe unaweza kuwaandalia mahesabu yao kwa gharama ambayo wanaweza kuimudu, unaweza kutengeneza biashara kwenye eneo hilo. Kama wewe ni mwanasheria unaweza kutoa huduma za kisheria kwenye jamii kwa gharama ambazo ni rafiki. Kwa mfano kuandalia wenye nyumba mikataba ya upangishaji, kuandalia wafanyabiashara wadogo mikataba ya uajiri, kuwaandalia watu mikataba ya kibiashara na kadhalika. Kuna taasisi nyingi zinafanya hivi lakini zinawafikia wateja wakubwa tu, wewe unaweza kuanza na wateja wadogo na ukajenga biashara yako hapo.
Kama unataka kuingia kwenye biashara hii ya huduma za kitaalamu, jua ile huduma ambayo unaweza kutoa na anza na wateja ambao hawajafikiwa na watoa huduma waliopo. Tengeneza jina lako kwa kutoa huduma nzuri na kuza biashara yako kuanzia hapo.
 Huduma za kitaalamu.
 
Blog unaweza kuitumia kwa biashara zote ambazo tumejadili hapo juu. Unaweza kuitumia kwa kutoa ushauri wa kitaalamu. Kama wewe ni daktari unaandika kuhusu mambo ya afya. Kama wewe ni mtaalamu wa rasilimali watu unaweza kuitumia kuandika kuhusu sifa za kuajiriwa, kudumu kazini, kupandishwa cheo na mengine mengi. Kupitia yale unayoandika unaweza kutengeneza hadhira ambayo inakufuatilia na baadae ukageuza blog yako kuwa biashara kwa kutoza huduma unazotoa, kuweka matangazo au kuuza vitu vyako vingine.
       Nakushukuru ndugu mpenzi msomaji nikushukuru kwa kuwa pamoja nami,usikose makala zingine tamu zinazoendelea kuandaliwa

No comments:

Post a Comment

NJIA ZITAKAZO KUJENGEA MSINGI MZURI WA MALI KATIKA UMRI WA 20+

Tabia zitakazo kusaidia kutumia na kutunza fedha kwa umakini,tabia hizi zitakufanya upate msingi bora utakapo fikia umri mkubw...