Tuesday, May 30, 2017

BIASHARA NDOGO ZA MAJUMBANI ZITAKAZO KUTOA KATIKA UMASKINI



JE WAJUA BIASHARA ZA MAJUMBANI  UNAZOWEZA KUANZISHA KWA MTAJI MDOGO?

                    Kama wewe ni mwajiriwa na umezichoka  kero na manyanyaso ya bosi wako,Je unahitaji kuwa bosi wako mwenyewe? Ungana nami katika makala hii uweze kuzijua biashara hizi ndogondogo zinazohitaji mtaji mdogo na kukupa faida kubwa.Wazo la kuanzisha biasharea majumbani ni wazo zuri linalopunguza gharama za uendeshaji na kukupelekea kunufaika zaidi.Biashara hizi hupelekea kupunguza tatizo la ajira pia husaidia wanawake kuepukana na unyanyasaji kutoka kwa waume zao.Badili muda wako wa kukuaa nyumbani kuzalisha kipato,Wazo la kuwa mwajiri wako mwenyewe ni jambo rahisi linalohitaji nidhamu ya hali ya juu sana ,kujituma na kujitambua.Kujiajiri nyumbani kuna faida nyingi kama kuepusha kupoteza muda barabarani,na gharama za nauli nk.Pia biashara hizi zinaweza kukusaidia kukuwezesha kulipia gharama za maisha kama vile kulipa kodi ,gharama za malezi nk.

Kabla ya kuanza biashara yako ya nyumbani kuna mambo mawili matatu ya kutazama

           Jambo la kwanza

 Fanya unachopenda.

Ili kuweza kumudu biashara yako nilazima uchague biashara unayoipenda.Jambo lolote unalopenda ndilo utakalolifanaya kwa moyo zaidi.Watu wengi waacha biashara kwa kuwa walifanya chaguo lisilo sahihi,hivyo kuwafanya kufanya pasipo bidii na uvumilivu pia,Jitahidi kutafuta biashara unayoipenda zaidi hitakusaidi kufanikiwa zaidi.

            Jambo la pili

 Je unayo mtazamo sahihi?.

Ili kufanikiwa ni lazima kuwa na mtazamo chanya wa jambo hilo.Mtazamo chanya hukupa nguzu za kufanya jitihada chanya kufikia malengo yako,jitahidi kabla yakuanza biashara yako uwe tayari kifikra na kimwili katika jambo hilo.Mtazamo chanya pia hukupa uvumilivu katika safari yako kuelekea katika mafanikio,hutakatishwa na kikwazo chochote.


             Jambo la tatu

 Kujenga mipango na mikakati ya kuanzisha biashara yako.

“Mali bila daftari huisha bila habari” msemo huo pia hutumika katika biashara,biashara ambayo haijaanzishwa kwa mipango na mikakati huanguka bila habari.Kabla ya kuanzisha biashara hakikisha unaijifunza kwanza biashara hiyo kabla,kwa kupitia vitamu na watu waliofanikiwa zaidi.Baada ya kufahamu biashara hiyo weka mikakati na mipango itakayokufanya kusonga mbele zaidi bila kukwama bila kusahau sheria na kununi bora zitakazo kuongoza wewe na pia kama hutaitaji wafanya kazi.


BAADA YA KUJIFUNZA HAYO KARIBU TUJIFUNZE BIASHARA HIZO ZA MAJUMBANI


Tutaanza moja moja kwa moja kujifunza biashara hizo yakwanza mpaka ya mwisho

            Kutengeneza na kuuza bidhaa za chakula

Kutengeneza bidhaa za kula majumbani pia mahotelini nk na kuuza mfano biskuti,keki,
Kupata mapishi yako favorite na kuuza, kama vile biskuti, vetkoek, koeksisters, muffins, keki, jams, crips nk huhitaji vifaa vichache na pia vya gharama ndogo vya mapishi.Biashara hii huitaji gharama ndogo ya kuanzia na pia bidhaa hizi huwa na wateja wengi kwa kuwa ni vya bei nafuu na hupendwa na watu wengi.Nikushauri na biashara ndogo ili kuweza kuimudu na kujenga faida kubwa mapema.

           Huduma za kompyuta/computer design.

Kama una kompyuta na vifaa vingine kama vile printer kamera nk,unaweza banzisha huduma za stetionary na kubandika vipeperushi vya matangazo ili kuvutia biashara.Biashara hii noi nzuri na hulipa pale unapokua karibu na shule au ofisi mbalimbali ambazo huhitaji huduma hizo,pia unaweza tengeneza kadi za sherehe na matukio mbalimbali.

         Kupiga picha
Kama unauwezo wa kupiga picha na tayari unayo kamera nzuri, unaweza kuajiri mwenyewe tofauti na kupiga  piga picha za harusi, matukio kama vile siku ya kuzaliwa.unaweza fungua studio yako nyumbani.


            Unaweza kuwa mwalimu.

Ualimu umegawanyika mara nyingi sana,unaweza kusoma fani fulani na kuanza kufundisha wanafunzi wako fani hiyo kama vile ushonaj,musiki na vingine kama hivyo,pia unaweza wafundisha fani nyingine ambazo unazo hata kama ujazisomea lakini unazimudu kama vile uchongaji au ususi.Unaweza jitolea kufundisha bure au kwa bei nafuu kwa muda ili kupata jina.


           Unaweza kua mshonaji.

Kama unauwezo wa kushona au kutarizi nguo na vifaa unavyo basi nkushauri uanze kutumia taaluma yako vizuri kwa kuanza kazi mapema mno,tumia uwezo wako wote katika kukamilisha jambo hilo.

Kituo cha kulea watoto (child care center).
Kwa sababu ya wazazi kubanwa na majukumu ya kila siku,huhitaji watoto wao wapate malezi.Baada ya matendo maovu dhidi ya watoto kuongezeka kupelekea wazazi kupeleka watoto wao  katika vituo hivyo.Kituo hichi ni rahisi kukianzisha kwa kua mahitaji yake ni machache na kukupa faida kubwa mno.



Ghala la kimtandao.(E-Commerce stores).

Unaweza anzisha wigo wa kimtandao mfano JUMIA ,ZOOM TZ,KUPATANA nk na  kuwapa fursa watu kuuza na kununua bidhaa kama vile magari,viwanja,nyumba,vitabu,mavazi  nk  kwa kuwatoza pesa ndo sana.Ndugu mpenzi msomaji naamini makala hii imekuasidia,mpenzi msomaji wangu nichukue nafasi hii kukushukuru nikuombe uendelee kubaki nasi pia usisahau kutoa maoni na kusambaza pia wengine wanufaike na elimu hii ahsante


Monday, May 29, 2017

Umasikini mpaka lini?




Mbinu hizi zitakusaidia kutoka

 

               Nijambo gani linalowafanya watu fulani pekee kufanikiwa?, jambo gani linalo wahamasisha?.
Vitu hivi vimenifanya kuandika makala hii ili kuwasaidia watu wenye nia ya kubadili maisha yao lakini hawajui wafanye nini.Zifuatazo ni mambo  yanayoweza kukufanya ubadili maisha yako pale tu utakapo zifahahamu.

UJIAMINI NA KUJIKUBALI.
                 Hiyo ni nguvu inayowafanya kusonga mbele kwa kua hujua thamani yao hiyo huwafanya kujiamini mno na kujikuli pia.Hilo  huwafanya kusonga mbele katika  mipango yao bila kukubali mtu yeyote kumrudisha nyuma au kumkatisha tama.

HUWA NA MALENGO, MADHUMUNI NA MAONO SAHIHI.
                     Maendeleo ya mwanadamu  huhitaji mikakati thabiti ili kuweza  kutekeleza mipango.Pale mwanadamu  anakosa malengo hujikuta akihangaika huku na huko bila kujua cha kufanya kipi,na hiyo humfanya kukosa au kuchelewa kuapata mafanikio.Malengo,madhumuni na maono sahihi humpeleka mtukwenye mafanikio moja kwa moja.
UTAYARI WA KUFANYA KAZI.
                     Watu wa mafanikio wana shauku ya kufanya kwa bidii zaidi.Tambua mafanikio huletwa na utayari wako kifikra na kimwili pia, bila kua tayari kufanya kazi kwa bidii unatemegemea kufanikiwa?Jibu ni hapana lazima ujitahidi kutoa mwili na akili yako kufanya kazi kwa bidii zaidi.

NIDHAMU.
                  Tambua mafanikio hujengwa na nidhamu ya halii ya juu lazima ujifunze kuheshimu wewe na mipango yako,jitahidi kujiagiza kuheshimu maagizo yako peke ako.

AKILI SHIRIKISHI.
                   Watu wanaohitaji kua na mafanikio lazima wawe na akili shirikishi au jumauishi  kati ya mawazo na akili zao.Huamini akili na mawazo yao .Unapokua na akili shirikishi ni lazima upate mafanikio kwa kua huwezi fanya jambo lilo nje ya mipango yako.

KUJIFUNZA  KWA FAIDA.
                     Kusoma kwa faida ni jimbo zuri sana kama unataka mafanikio ya haraka,kwa kusoma huko hukupa elimu unayoitaka kukusaidia kutimiza mipango yako.Mfano unahitaji kufuga kuku wa nyama ni lazim  husome na kufuatilia haytua kwa hatua kanuni za ufugaji bora.Bila kujifunza kwa faida huwezi timiza ndoto zako.

KUJITAMBUA
                    Kujitambua ni hatua mojawapo kubwa ya mafanikio,ili kupata mafanikio ni lazima hujue wewe umekuja Dunini kufanya nini.Hukifanya jambo ambalo unalipenda jua utafanya kwa moyo zaidi na kupata mafanikio zaidi ,kwa  msaada kujitambua wewe ninani bofya hapa >> UNADHANI WEWE NI NANI? 


 Asante kwa kua nami katika makala hii tukutane tena katika makala zingine



Saturday, May 27, 2017

UNADHANI WEWE NI NANI? WHO YOU ARE?



UNADHANI WEWE NI NANI?
KUWA ULIVYO NI MUHIMU KULIKO KUWA WATU WANAVYOTEGEMEA UWE




JE UNAISHI KWASABABU YA KUA MWALIMU?

JE UNAISHI KWAAJILI YA KUFANYA BIASHARA YA MATANGAZO?

JE UNAISHI KWASABABU YA KUWA MUONGEAJI WA HADHARA?

JE UNAISHI KWA AJILI KUA MWANDISHI MWENYE MAFANIKIO?

JE UKO KWA AJILIMYA KUA MUUGUZI?

JE UNAISHI KWA AJILI YA KUWA MWALIMU?

JE UNAISHI KWA AJILI GANI?
 JICHUNGUZE TAMBUA KIPAWA CHAKO,KUSUDI LAKO KUISHI
         "Kipawa ni kama silaha aliyopewa mwanadamu kumwezesha kuishi  katika mazingira yanayomzunguka",Kipawa humsaidia mtu binafsi pia huwasaidia watu wengine.
          Kila mwanadamu anayeishi chini ya mbingu hii anacho kipawa chake alizaliwa nacho  kufanikiwa katika dunia,ili ,tu kufanya jambo kubwa katika maisha nilazima kutumia kipawa chake vyema,kama hukifahamu kipawa chako ni rahisi kufanikiwa katika jambo hilo hunalokusudia kwakua ndo wajibu wako katika dunia.
        Mwanadamu yeyote ni bora na wamafanikio kama atakitambua kipawa chake na kukitumia,hakuna kipawa kidogo na kikubwa vyote ni sawa tatizo huja katika juhudi za kukiendeleza hicho kipawa.
        Katika kazi ngumu huwa ni kujaribu kufanya jambo.Nakufanya jambo huletwa na mawazo sahihi,je kuwaza mawazo chanya ni jambo rahisi? "nadhani hapana" watu wengi hukwepa kuwaza fikra sahihi kwa mfano mtu huangalia muvie siku nzima je si njia ya kukwepa kufikiria mwazo chanya?.
       Ndugu mpenzi msomaji nikushauri usikate tamaa katika kuendeleza kipawa chako na usikidharau jitahidi kulifanya kusudila lako kuishi,na pia kama bado hujakitambua kipawa chako jaribu kutafakari kila unapopata muda utagundua kusudi lako siku moja usikate tamaa,nikuombe endelea kusoma  makala hizi Mungu akubariki sana





NJIA ZITAKAZO KUJENGEA MSINGI MZURI WA MALI KATIKA UMRI WA 20+

Tabia zitakazo kusaidia kutumia na kutunza fedha kwa umakini,tabia hizi zitakufanya upate msingi bora utakapo fikia umri mkubw...